💥 Njia Rahisi ya Kuzuia Matangazo kwenye Simu Yako
Kama unataka kuzuia matangazo bila kufanya root, tumia Private DNS. Hii ni moja ya njia bora na rahisi.
Jinsi ya Kuzuia Matangazo kwa Private DNS:
- 1️⃣ Nenda Settings kwenye simu yako.
- 2️⃣ Fungua Network & Internet (au Connections kwenye baadhi ya simu).
- 3️⃣ Bonyeza Private DNS.
- 4️⃣ Chagua Private DNS provider hostname.
- 5️⃣ Andika: dns.adguard.com
- 6️⃣ Bonyeza Save.
Matokeo:
Matangazo mengi kwenye apps na browser yataondoka bila kuhitaji root wala programu nyingine. So kama ads zinakuletea noma, nenda kazipunguze🏃🏽♂️🏃🏽♂️
