TAFAKARI
Mbwa alikuwa mwaminifu sana kwa mwanamke huyu kiasi kwamba alikuwa akimuachia mtoto wake na kwenda popote alipohitaji. Mara zote alirudi na kumkuta mtoto wake amelala fofofo mikononi mwa mbwa. Siku moja jambo la kusikitisha lilitokea.
Mwanamke huyo, kama kawaida, alimuacha mtoto mikononi mwa mbwa huyu mwaminifu na kwenda sokoni.
Aliporudi, aliona tukio la kutisha, na kulikuwa na msiba mkubwa. Mtoto hakuwepo kwenye kitanda chake, nep na nguo zake zilikuwa vipande vipande, huku kukiwa na madoa ya damu chumbani kote. Kwa mshtuko, mwanamke aliyeogopa alianza kumtafuta mtoto. Mara akamuona Mbwa mwaminifu akitoka chini ya kitanda, akiwa ametapakaa damu kila mahali akiramba mdomo wake kana kwamba alikuwa amemaliza kula chakula kitamu.
Mwanamke huyo alikuwa na hakika kwamba mbwa alikuwa amemla mtoto wake. Bila kufikiria sana, alimpiga mbwa kwa ukuni mpaka kufa. Ndipo uchunguzi ukaendelea angalau kupata mabaki ya sehemu ya mwili wa mwanae.. Nyuma ya kitanda kulikuwa na mtoto huyo ambaye alikuwa uchi na akicheza cheza kwenye kapeti, Chini ya kitanda... Pia mwanamke huyo aliona mwili wa nyoka aliyekuwa amepasuliwa vibaya. Ilikuwa vita vikali kati ya nyoka na mbwa. Mbwa alipigana ili kumlinda mtoto asidhuriwe na nyoka mkali. Alikuwa amechelewa sana kurejesha amani kwa sababu ya kukosa subira na hasira, alikuwa amemuua mbwa mwaminifu ambaye hakuwa na kosa lolote.
Ni mara ngapi tunawahukumu watu kwa maneno makali na kueneza uongo kuwahusu kabla ya kuchukua muda wa kutathmini athari zitakazojitokeza? Pata muda wa kuchunguza kabla ya kufanya maamuzi.. Unaweza mpoteza mtu au kitu cha thamani kwa sababu ya kutofikiria kwa kina.. Wahenga walisema FIKIRI KABLA YA KUTENDA..
"Mara zote kuwa na subira na epuka makosa ambayo yanaweza kukuangusha."
Uwe na siku njema.
