Ili kuzuia WhatsApp yako isiwe hacked, fuata hatua hizi za usalama:

Njia Bora za Kulinda WhatsApp Yako

Njia Bora za Kulinda WhatsApp Yako

Hakikisha unafuata hatua hizi ili kulinda akaunti yako ya WhatsApp dhidi ya wadukuzi na udukuzi wa taarifa zako binafsi.

1. Washa Two-Step Verification

Fungua WhatsApp na nenda kwenye Settings > Account > Two-step verification.

Weka PIN ya usalama na email ya kurejesha.

2. Usishiriki OTP (One-Time Password)

Usimpe mtu yeyote msimbo wa uthibitisho unaopokea kwa SMS.

3. Tumia Fingerprint Lock au Face ID

Android: Settings > Privacy > Fingerprint lock.

iPhone: Settings > Privacy > Screen lock.

4. Epuka Linki na Programu za Ajabu

Usibonyeze linki zinazotumwa na watu usiowajua.

Usipakue WhatsApp kutoka kwa tovuti zisizo rasmi.

5. Angalia Active Sessions (Kama Mtu Anatumia WhatsApp Yako Kwingine)

Fungua Settings > Linked devices.

Kama kuna kifaa usichotambua, bonyeza Log out.

6. Sasisha (Update) WhatsApp Mara kwa Mara

Hakikisha unatumia toleo jipya kutoka Google Play Store au App Store.

7. Epuka Public Wi-Fi bila VPN

Public Wi-Fi inaweza kutumiwa kudukua data zako.

8. Hakikisha Simu Yako Ina Antivirus

Inasaidia kuzuia spyware na malware ambazo zinaweza kuiba taarifa zako.

Je, WhatsApp Yako Imehacked?

Kama unashuku WhatsApp yako imehacked, unaweza kuisajili tena kwa kutumia namba yako ili mtu mwingine atoke.

#bright life with us

Post a Comment

Previous Post Next Post